STORY: HISTORIA BATILI
MTUNZI: JUMAA KHATIB MDHARUBA
+255718274130
EPISODE 13
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Siku ya Jumapili asubuhi, ndiyo siku iliyopangwa kufanyika arubaini ya Sauda..
Watu wengi walikusanyika kwa ajili ya shughuli ile ambayo ilipangwa kufanyika ndani ya masaa mawili tu, saa 2:00 mpaka saa 4:00 asubuhi. Kitu kilichowashangaza wengi hapa ni kutoonekana kwa Khatib, mume wa marehemu..
“Mama, Khatib hatoweza kufika leo, mimi nitakuepo nikimuwakilisha hapa” Kwa sauti ya upole Hisham aliongea kumwambia Mama wa Marehem, Mama Sauda..
“Mmmmh, unasemaje? Yaani wewe ndo umuwakilishe Khatib, yeye mwenye mkewe? Nyie mbona siwaelewi? Sasaaa...duuuh...jaaamaaniii..akili gani hizi.!? Yaani mtu uwakilishwe kwenye msiba wa mkeo? Mmmh Makubwa haya..ndo kwanzaa leo naona..”
“Yeye mwenyewe kaenda wapi kwani?”
“Amesafiri” Hisham alijibu kifupi.
“Jaamaanii..hivi mnajua nyie mnachekesha sana, sasa mtu anasafiri vipi katika hali hii kweli?” Mama Sauda alizidi kushangaa..
“Kwani wewe mama unatakaje?” Alihoji Hisham ambaye alikua mwepesi sana wa 'kupanic'..hapa alishachoshwa na maneno ya huyu mama..
“Basi mwanangu, tuangalie haya kwanza” aliongea mama Sauda baada ya kuona hali ya Hisham, alishagundua kuwa hakukuwa na kher tena katika yale mazungumzo..akaona busara ni kuyakatisha tu..
Shughuli iliendelea vizuri na hatimaye wakamaliza salama, kila mtu aliyekuwepo akishangazwa na tukio la Khatib kutohudhuria kwenye shughuli ile ya marehemu mke wake..Umaarufu una matatizo yake, hiyo ilibaki mada kwa muda mrefu katika vinywa vya watu. Hapa ndipo zile habari za chinichini zilianza kusambaa kwa haraka kama moto wa petrol..Khatib amemuua mkewe..na watu wengi wakihusisha na tukio la Kulwa kutaka kupima mwili wa marehem wakati ule wa msiba..Kifupi ni kuwa maneno yalikua ni mengi..Ila watu walisema wao tu, hakuna aliyekua na ujasiri wa kwenda kuhoji, unaanzia wapi? Maana wapambe wa Khatib wote walikua wakijulikana kuwa ni watu wababe..na kama Khatib ameweza kumuua mkewe aliyekua akilala nae kitanda kimoja atashindwa kukuua wewe unayejifanya kimbelembele?!
“Wazee, tunashukuru tumemalizia msiba salama, kila kitu kiko vizuri Alhamdulillah, kilichobaki hapa ni kumsubiri huyu bwana arudi ili tuweze kuangalia taratibu za mirathi zinaendaje, maana Sauda alikua na vitu vyake vingi tu pale nyumbani” Aliongea Hisham kwa niaba ya Khatib kama alivyoagizwa kabla Khatib hajasafiri..
“Sawa, hakuna shida..tuombe kheri tu..” Aliongea Mzee J4 ambaye ndiye aliyeteuliwa kuwa msemaji wa familia katika shughuli hii..
Baada ya hapo wakafunga kikao hiki kifupi, kisha kila mtu akaanza kutafuta pa kuelekea.
Wakati anatoka nje, ghafla Hisham alijikuta akishtuka baada ya kukamatwa mkono wake wa kushoto na Mzee J4.
“Naam Mzee kwema?”
“Kwema tu kijana wangu, si unaelekea kwenye gari yako?”
“Ndio”
“Twende pamoja kuna kitu nataka tuongee kidogo”
Hishama akaanza kupatwa na wasiwasi, hakujua Mzee J4 anataka kuongea nini, hili ndo tatizo..na Mzee huyu alishaonesha dalili kuwa yuko makini sana katika mambo yake..alikuwa na upeo.
Walifika kwenye gari, Hisham akafungua mlango wake upande wa usukani, akiruhusu na Mzee J4 afungue mlango wa upande wa pili na kuzama ndani.
“Ndio mzee tunaweza kuendelea sasa..”
“Nyie vijana wadogo sana, lakini mna matatizo makubwa.. 'Power' haina mwisho, hata uitawale dunia, bado utatamani uwe na 'power' zaidi ya hapo..tumeshuhudia machafuko na vifo vingi sana duniani, vyote vikitokana na watu wa aina kama yenu wanaotafuta 'power'.. Sasa mtaua wangapi? Mtawafunga midomo watu wangapi kama mlivyofanya kwa Kulwa mpaka kashindwa kuhudhuria arubain ya mdogo wake?.. Mnavyovitafuta bado hamjapata tu? Khatib ana miaka 27 tu, lakini anafikia hatua ya kuua kwa sababu ya 'power'??” Mzee J4 alikuwa akifunguka mbele ya Hisham ambaye muda huu alikua haamini anachokisikia masikioni mwake..
“Mwambie huyo mwenzio akirudi anitafute nina maongezi nae marefu, USIPUUZE” Ndivyo alivyomalizia Mzee J4 akafungua mlango na kurudi nyumbani kwa dada yake.
Hisham alibaki ameduwaa pale kwa dakika kadhaa..hajui cha kufanya..haamini kuwa Mzee J4 anaweza kuyaeleza yale yote kwa kujiamini kiasi kile..
“Mmmh hawa wazee wengine nuksi sana, duuh..mwaka umeanza vibaya huu...kama na mimi nisingempa mafasi Regina akaendelea kuishi si tungeonekana wazi kuwa sisi ni wauwaji?” Aliwaza Hisham..
Kabla hajaondoka eneo lile alionekana kukumbuka kitu, akachukua simu yake akabofyabofya kisha akaweka sikioni..
“Hallooo..bila shaka naongea na Hamida” alianza kuongea Hisham sekunde 20 baada ya kuweka simu sikioni..
“Ndio, nani mwenzangu?”
“Naitwa Hisham Omari Mikidadi, manager wa Mambo pub, rafiki mkubwa wa Mr Khatib”
“Oooh oky..sawa”
“Khatib aliniachia namba yako kabla ya kusafiri..nahitaji kuonana na wewe nina ujumbe wako”
“Sawa..hakuna shida, kama upo Tanga njoo nyumbani.” Hisham akaendesha gari kutoka eneo la msiba mpaka nyumbani kwa kina Hamida safari iliyomaliza takriiban dakika 12 mpaka kufika.
Alipofika nje alishangaa kidogo kuona wako 'busy' wakijiandaa kutoka..
“Vipi tena? Nini tatizo?”
“Hali ya Abdul sio nzuri.. Amezidiwa sasa hivi ghafla ndo tunaelekea hospitali hivi..” Alijibu bi Nana ambaye alkuwa anamalizia kufunga duka muda huu..
“Basi tutumie gari langu ili tumuwahishe”
“Ok, sawa baba Ahsante sana”
Wote watatu pamoja na Abdul wakaingia kwenye gari kuelekea hospitali..
“Vipi kwani nini kimetokea” aliuliza Hisham wakati safari inaendelea
“Mimi hata sijui..ila ameanguka ghafla tu huyu mtoto, sijui nini tatizo” Hamida alitoa jibu hili huku sauti yake ikiwa haisikiki vizuri sababu ya kilio
******************************
“Tumefanya vipimo vya awali, mtoto ana upungufu mkubwa wa damu..hivyo anatakiwa aongezewe damu..” Alisema Dr Elisha Singano, daktari wa magonjwa ya watoto katika hospitali ya mkoa..kisha akaendelea..
“Sisi hapa hatuna akiba ya damu, kwahiyo aje mmoja hapo aliye tayari tuchukue vipimo ili aweze kujitolea damu..” Baada ya maelezo haya ya Dr Elisha, Hisham ndiye alikuwa wa kwanza kunyanyuka kutoka katika benchi walilokuwa wamekalia moja kwa moja akaongozana na Dr Elisha..
Akafika na kufanyiwa vipimo vya HIV na 'blood group' kisha baada ya muda Dr Elisha akatoa majibu..
“Mr Hisham Omar, Nasikitika kukwambia kuwa huwezi kumchangia damu mgonjwa”
Akaweka nukta ndogo Dr Elisha, Hisham kijasho chembamba kikimtoka, akaanza kufikiria wanawake wote aliowahi kupita nao katika maisha yake, wale aliopiga kavu na hata aliotumia condom..machozi yakaanza kumtoka..akamwangalia Dr Elisha ambaye alionekana bado anaendelea na maelezo yake..
“Damu yako ni safi, haijaathirika isipokuwa wewe kundi lako la damu ni AB wakati mgonjwa wetu yeye ni kundi O (blood group O) ambaye hawezi kupokea damu ya group nyingine yoyote zaidi ya O.” Alimalizia maelezo Dr Elisha na kumfanya Hisham ashushe pumzi ndefu..
“Naomba uharakishe umuite mamaake pengine damu yake yaweza ikafaa..”
Hisham akatoka na kumuita Hamida akimuelezea tofauti za magroup ya damu kati yake na Abdul..
“Duuh kama ni hivyo kazi ipo, ngoja mimi niende nokajaribu” Akasema Hamida na kuzama chumba cha daktari.
******************************
“Vipimo vinaonyesha wewe ni blood group A with Rhesus positive(A+) kwahiyo pia damu yako haiwezi kupokelewa na mgonjwa..” Maneno haya ya Dr Elisha yalikata maini ya Mama Abdul, akaanza kutokwa na machozi..
“Mwite bibi yake mtoto, huenda akasaidia..” Dr Elisha alimnasihi Hamida baada ya kumuona amekata tamaa..
“Hapana Dokta, mama pia hawezi kusaidia, sababu tulishawahi kwenda hospitali moja zamani nilimchangia damu, Dokta alituambia mimi na mama tuna group sawa za damu..ila kwa kipindi hicho nilikua sijui ni group gani..kwahiyo kama umepima na ukaona nina A+ basi na mama ana hiyohiyo..” Aliongea Hamida akiwa analia kwa kwikwi, akifikiria hatma ya mwanae wa pekee..Abdul..aliwaza mengi saaana..mipango yake kuhusu elimu ya mwanae huyo, akiona mwanzo mzuri kwani babaake kwa sasa alishaanza kuonesha nia ya kuishi pamoja nae..
“Sasa kama kuna ndugu yeyote wa karibu mpigie basi simu aje aokoe jahazi..kwa sasa kulia sio jawabu la tatizo hili” Dr Elisha alimnasihi Hamida..
Hamida alifikiria kwa kina, kabla hajatoa jibu lolote Dr Elisha akauliza swali ambalo lilitoa mwanga katika akili ya Hamida..
“Kwani babaake mtoto yuko wapi? Maana yule Hisham amenambia yeye sio baba wa mtoto..”
Baada ya swali hili Hamida akamwangalia Dokta Elisha saana..akikumbuka maneno ya Khatib aliyokuwa akiyatamka mara kwa mara kipindi cha uhusiano wao..“Sisi wenye damu group O nadra sana kuumwaumwa..hii ni damu adimu sana..”
Kisha akanyanyuka kutoka katika kiti alichokua amekaa..
“Subiri kidogo Dokta”
Akafungua mlango na kutoka..
“Hisham, ulisema baba Abdul amekupa namba yangu unitafute kabla hajasafiri, kwani ameelekea wapi?” Ni swali aliloanza nalo kwa Hisham ambaye alikuwa amejiinamia akitafakari cha kufanya
“Canada” alijibu Hisham kwa kifupi sana..
Hamida akaanguka na kupoteza fahamu.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Be patient, wait for Episode 14..
Whatsapp↘
+250726023140
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni