STORY: Historia Batili(Fake History)
MTUNZI: Jumaa Khatib Mdharuba
+255 718 274 130
+255 719 274 130
+255 756 274 130
+255 779 274 130
mdharuba@gmail.com
www.facebook.com/khatibj
IG: Sir_mdharubajk
EPISODE 12
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Ilikua tarehe 5 Mei, siku ya kuzaliwa ya bi Nuro Ahmed, mama aliyehusika kwa asilimia zote kumtafutia mke wa kuoa Mr Khatib, na mwishowe akampendekeza Sauda ambaye ndiye alikuwa mke wa Khatib kwa miaka miwili hii..Siku hii Nuro aliamka mapema sana, akawahi pale kituoni kwake wanapolea watoto, aliamua kwenda mapema kuliko kawaida kwani siku hiyo alitaka akawaage na asikae sana ili akasherehekee siku yake ya kuzaliwa na Mumewe kipenzi Mr Feisal..
Hata hivyo alipanga apitie tena pale kituoni baadae ili aungane na watoto wale pamoja na wale walezi wengine ili wale pamoja keki waliyoiandaa kwa ajili ya sherehe hiyo ya kuzaliwa..
Lakini kabla hajaondoka pale kituoni akakumbuka kitu, akatoa simu iliyokuwa katika mkoba wake mweusi ambao alikua hajautoa kwapani muda huo, akabofyabofya namba fulani kisha akaweka sikioni.
“Haloo..Assalaam alykum..”
“Waalykum salaam dada..vipi hali?”
“Hali yangu nzuri tu, ila nataka kukuuliza kitu kimoja..” Alianza kuongea Nuro moja kwa moja kwenye 'point' pasipo kurefusha salamu kama ilivyo kawaida yake..
Mr Khatib, ambaye aliipokea simu hii ya Nuro kwa kujiamini ingawa ilimshtua, alivyosikia hivi akili yake ikamtuma moja kwa moja kuwa Nuro alitaka kuulizia juu ya kifo cha Sauda.
“Ni muda mrefu sasa hujanitafuta, na pia nilitegemea taarifa ya kifo cha Sauda wewe ndio uwe wa kwnza kunipa, ila naona kimya tu, mpaka leo nimeambiwa kuwa 40 yake ni Jumapili, wewe una matatizo gani ndugu yangu? Mbona nashindwa kukuelewa?” Bi Nuro alianza kumtupia lawama Mr Khatib, lawama ambazo zilimstahili haswa.
“Naomba unisikilize kwa makini dadaangu, niskilize kwa makini sana ili twende sawa..” Alianza kuongea Mr Khatib, hapa akijaribu kutaka kupata pa kuanzia..
“Hivi unafikiri ni jinsi gani mi nimechanganyikiwa baada ya kumpoteza mke wangu kipenzi Sauda? Unajua niko katika hali gani mpaka sasa? Mi nilitegemea hata baada ya kupata taarifa wewe ndo uwe mtu wa kwanza kunifariji, leo hii wewe unakuja kunitupia lawama kiasi hiki kweli? Au labda umenichukuliaje? Mbona Nuro ni tofaut na ninavyokufikiria? Kwahyo wewe umeamua kunilaumu kwa mimi kupoteza mke wangu? Ok sawa..” Alimalizia hivyo Mr Khatib kisha akakata simu.
Nuro alijaribu kupiga ile simu mara nyingi baada ya kukatwa, lakini simu haikua ikipatikana!!
“Hii ndo kawaida ya watu wahalifu, sasa naanza kuamini kile alichonambia Ahmed” Alijisemea moyoni bi Nuro.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Captain, naanza kuamini maneno yako sasa, huyu Khatib huenda akawa amemuua mke wake” Alisema bi Nuro baada ya kumpigia simu Ahmed Khamis ambaye kwa vyeo vyao vya kazini Ahmed alijulikana kama 'Captain'.
“Nipo katika hatua za mwisho za uchunguzi wangu Senior, nikikamilisha utapata taarifa kamili, ila hilo jambo mimi nina uhakika nalo siku nyingi tu, huyu bwana ni muuaji tu, na ipo siku tutamtia ndani ya mikono ya sheria” Aliongezea maelezo ya Nuro bwana Ahmed, ambaye na yeye alimtambua Nuro kama 'Senior'.
Kabla ya kukata simu, Nuro alimkumbusha Ahmed kitu..“Usisahau kumjulisha Detective kuhusu hili jambo, maana aliniuliza leo asubuhi wakati nampa ripoti ya lile tukio la yule binti aliyekuwa akijifanya mlemavu wa masikio hapa kituoni”.
“Ok, nitafanya hivyo, ingawa napendelea zaid kuongea na Detective nikiwa nimekamilisha kila kitu, ila ntampigia”
Baada ya mazungumzo haya, Ahmed aliondoka kutoka katika kivuli cha mti wa muarubaini pale shuleni, mti uliokua mbali kidogo madarasa, ambako alikua akipatumia sana kuongea simu hizi za siri..moja kwa moja akarudi ofisini.
******************************
Nuro Ahmed, alikua ni afisa Usalama wa taifa kama vile alivyo Ahmed Khamisi, ingawa walitumwa kwa kazi tofauti mjini Morogoro, bali Rukia Akida Sembony ambaye walimtambua kama 'Detective', ambaye ndiye bosi wao mkuu na anayewapangia kazi za kufanya kwa mujibu wa maelekezo anayoyapata yeye kutoka makao makuu, alipenda washirikiane katika baadhi ya kazi ambazo zilionekana ni ngumu kwa mtu mmoja kuzimudu..
Mama yake Khatib, mama Mdharuba alikuwa na uhusiano mzuri sana na Nuro Ahmed, lakini hakuwa akifahamu kuwa Nuro anashirikiana na Ahmed katika kazi maalum ya kumchunguza kwa undani mwanae Khatib, ambaye kiusalama walikua 'hawamuelewi'.
Nafasi pekee muhimu ambayo Nuro aliipata ni kupewa nafasi ya kumchagulia mke Mr Khatib, aliifurahia sana nafasi hii..kwa sababu ilikua ni nafasi ya pekee ambayo Nuro angeweza kuweka kibaraka wake ndani ya nyumba ya Khatib..
Nuro alimpendekeza Sauda kwani ndiye mtu pekee aliyekua akimsikiliza kwa kila jambo pale kituoni kwao, hivyo aliamini kwa uwepo wa Sauda katika nyumba ya Khatib kungerahisisha sana kazi hii ambayo yeye(Nuro) na Ahmed waliifanya kwa umakini mkubwa mno.
Sauda, licha ya kuolewa na Khatib, hakuwa akijua kuwa alipendekezwa kwa yule mume kwa lengo maalum, yeye mwenyewe akijua ni kwa sababu ya tabia zake tu ndio maana akapendekezwa kuolewa na mtu tajiri kama Khatib, aliifurahia nafasi ile na akazama kwenye mapenzi mazito kwa mtu yule 'hatari' bila yeye mwenyewe kufahamu.
Nuro alikuwa akimtumia sana Sauda enzi za uhai wake kupata 'infornation' mbalimbali zinazomuhusu Khatib, Sauda yeye alifunguka moja kwa moja kwa maswali aliyokuwa akiulizwa na Nuro ilhali hajui nini kinaendelea nyuma yake. Ingawa Nuro alikuwa akihoji maswali mengi sana juu ya Khatib, lakini alikuwa hajapata maelezo ya kuridhisha sana ndani ya miaka yote miwili kwani Sauda alikuwa haonekani kujua vitu vingi kuhusu Khatib.. Khatib alikuwa msiri!! Na hili alilimudu.
“Captain, nini unafanya muda wote huu? Kwanza ni muda mrefu sijapokea ripoti yako..sielewi umefikia wapi..Mbona kama unaonekana kazi imekushinda?!” alihoji bi Rukia 'Detective' ambaye alishakuwa na wasiwasi juu ya 'ukusanyaji data' wa Ahmed..
“Naomba siku 3 tu Detective..kila kitu nitakiwasilisha katika mikono yako” Aliomba nyongeza ya muda Ahmed, ingawa hakuwa na uhakika wa kukamilisha hiyo kazi ndani ya siku hizo tatu alizoomba.
“Work hard” Ndivyo alivyoaga Detective Rukia.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Hapa kazi ipo..huyu mtu pengine ana zaidi ya ninavyomfahamu mimi, kuna uwezekano mimi nikaja nikawa katika wakati mgumu zaidi mbeleni kuliko yeye..” Aliwaza Hisham Omari Mikidadi baada ya kuambiwa kile ambacho aliambiwa ni siri na Mr Khatib..
Alifikiria maelezo yale aliyopewa kwa siku nzima, hata usiku alishindwa kulala..
Mkewe Hisham, bi Regina Madaba, aligundua tofauti iliyokuepo usiku huu wa leo kwa mumewe..kwa mara ya kwanza alimshuhudia Hisham akikosa usingizi..
Regina ambaye alifahamiana na Hisham kwa zaidi ya miaka saba sasa, tangu wakiishi kama wapenzi mpaka walipoamua kwenda kuandikisha mkataba wa ndoa serikalini ili waishi pamoja, alimfahamu vizuri sana mumewe..
“Mume wangu, mi naona mwanzoni ulikua katika hali nzuri zaidi ingawa ulikua katika biashara haramu ya unga, ila kwa sasa umeingia pabaya zaidi kwakuwa unashirikiana na Khatib, yule sio mtu mzuri..na kama utaendelea kushirikiana nae mimi sioni mwisho mzuri..” aliongea Bi Regina ambaye alikuwa anaongea maneno haya huku amemshika bega mumewe ambaye alikua amegeuka upande wa pili akiyasikiliza maneno haya ya Regina kutoka sikio lake la kushoto..
Hisham baada ya maneno haya ghafla alimgeukia Regina na kumuangalia huku amemtolea macho kisha akamuuliza..
“Unasemaje wewe mpuuzi??!!”
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Episode 13 coming soon..
Maoni: +255 718 274 130
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni