STORY: HISTORIA BATILI
MTUNZI: Jumaa Khatib Mdharuba
+255718274130
www.mdharubajk.blogspot.com
EPISODE O14
1⃣4⃣
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Ni takriiban wiki ya saba sasa, Nira Saire akiwa bado na hali mbaya kitandani..Mwenyewe alikua akiamini kuwa sasa ni zamu ya kuondoka duniani baada ya kutembea na virusi vya Ukimwi(HIV) kwa zaidi ya miaka 15 sasa.. Ndio, alihisi hastahili kuwepo tena duniani..
Pamoja na yote aliyoyafanya huko nyuma, lakini duniani alimchukia sana mtu mmoja tu-Regina Madaba, mke wa Hisham, ambaye ndiye yeye aliyemtambulisha kwa Jessica msichana aliyemwambukiza HIV.. Regina ambaye kabla ya kukutana na Hisham alikua akimiliki danguro la machangudoa maeneo ya Itigi Morogoro, alikua akimfahamu Nira kwa mara ya kwanza wakikutana kwenye basi wote wakitokea Dar kuelekea Moro..kutokana na muonekano wa Nira, Regina aliona huenda akawa mteja wake mzuri kwa kazi yake ile iliyokuwa ikimuingizia kipato na kumuweka pale mjini..!!
Baada ya kuchukua namba za simu za Nira kabla hawajafika stendi kuu ya mabasi ya Msamvu Morogoro, Regina alikua akiwasiliana na Nira mara kwa mara mpaka hapo walipozoeana sana na kumtambulisha Nira kwa Jessica msichana ambaye ndiye alionekana 'classic' zaidi kuliko wote waliokuwa wakijiuza katika danguro lile..
Nira akawa 'anatoka' na Jessica kwa mara zisizo idadi..mpaka akawa kama mkewe haswa..
Kwa upande wa Jessica yeye alishajua kuwa ni mwathirika siku nyingi sana..na Nira yeye alifikia 'stage' akamuamini sana Jessica mpaka akawa hataki hata kutumia 'condom' wakiwa 'wanafanya yao'. Jessica yeye hakujali sana kwakuwa alishajikatia tamaa ya maisha siku nyingi, yeye kwake mtu akitumia kinga na asipotumia ni sawa tu..
Pamoja na kuathirika, lakini Jessica ni yeye pekee ndiye aliyejua habari ile. Hakuwahi kumwambia mtu yeyote zaidi ya kukaa nalo jambo lile moyoni mwake, hivyo hata Regina hakuwa akifahamu kuhusu kuathirika kwa Jessica.
Nira hakuchukua muda mrefu sana kugundua kuwa ameambukizwa virusi vya Ukimwi kwani alikuwa na kawaida ya kucheki afya yake mara kwa mara..
Alianza kumchukia Jessica, kisha alipoona haina tija hasira zote akazihamishia kwa Regina akiamini kuwa Regina anajua kuhusu Jessica ila aliamua kumtumbukiza pale makusudi.
“Nitafanya kila namna nihakikishe na yeye anapata hivi virusi, tugawane maumivu...na nitamuambukiza mimi mwenyewe”. Ndiyo yalikua mawazo yake Nira baada ya kufikiri kwa muda mrefu sana, hiyo ndio ilikua 'conclusion' yake.. Alimchukia Regina kutoka moyoni lakini pasipo kumwambia..
*******************************
Nira alifanikiwa 'kupiga show' mbili tatu na Regina baada ya juhudi za muda mrefu akimshawishi Regina kuwa baada ya mwanafunzi kushuka kiwango sasa anamtaka mwalimu wake kwa gharama yoyote ile..Akatajiwa 'dau' akagharamia na akaanza 'kumega mzigo' katika hali ambayo inaeleweka haswa..
Regina naye alijisahau sana katika jambo zima la condom na kufanya Nira kushangilia ushindi kimyakimya..
*********
Kwa kipindi chote cha Nira kuumwa na msiba wa Sauda..kampuni ya Saukhat Inv Inc..ilikuwa chini ya kijana Fred Moshi, ambaye ndiye aliyekuwa akiaminika zaidi na mwenye upeo baada ya Nira..na maisha ya pale yaliendelea vizuri kwani Fred aliijua haswa kazi yake..
Licha ya Khatib kutaka kuifunga kampuni kwa muda kabla hajasafiri, lakini alijikuta akiahirisha maamuz yake baada ya kuona jinsi Fred anavyoiendesha kampuni..alikua makini mno, na hesabu zilikua zikija vizuri zaidi hata ya anavyotoa Nira ama Marehemu mkewe..
Fred akapewa madaraka ya kuendelea na kuiendesha kampuni.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Kuna mwanamke mmoja raia wa hapahapa Canada nahisi kuna jambo atakua anashirikiana nae, ngoja nimfuatilie kwa siku hizi atakazokuwa huku ili nikamilishe ripoti kamili Detective” Ndivyo alivyokuwa akitoa maelezo Ahmed kwa Detective Rukia, baada ya kupanda ndege moja na Khatib akiwa anakamilisha uchunguzi wake ili amjue Khatib kwa undani haswa kabla ya kulikabidhi kazi jeshi la polisi ili limtie katika hatia..Khatib yeye mpaka muda huu alikua hajajua kama anafuatiliwa.
“Sawa kazi njema” Ndivyo alivyojibu Detective na kukata simu..
★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Ngoja nifanye mawasiliano na Mama nitakutafuta ASAP”
Hisham ambaye alikuwa amekosa la kufanya alisoma ujumbe huu uliotumwa kupitia barua pepe yake na Khatib dakika chache tu baada ya kumtumia ujumbe akimueleza situation ilivyo pale hospital..
Wakati bado akiwa kwenye dimbwi la mawazo huku akifikiria zaidi hatma ya Mama Abdul ambaye alianguka na kupoteza fahamu mbele yake, simu yake ikaita.. “Magic_Princess” ndiye alikuwa mpigaji..
“Baby..ni muda mrefu sasa umepita naona kimya, maana ulinambia shughuli inaisha saa nne na sasa inakimbilia saa nane hii, vipi kwani kuna tatizo mpenzi?” Ndivyo alivyoanza Regina, ambaye alikuwa ameongozana na Hisham wote wakija Tanga, ila walikubaliana kuwa Hisham aende kwenye shughuli ile ya arubain huku Regina akitumia muda huo kwenda kuwasalimia ndugu zake ambao walikuwa ni wengi sana Tanga mjini pale kwani Mamaake Regina alikuwa ni mzaliwa wa hapo.
“Yaah tatizo lipo, nimechanganyikiwa ndio maana nimeshindwa kukutafuta mke wangu..”
“Heee..kuna tatizo gani tena hubby?”
“Naomba uchukue pikipiki uje hapa hospitali ya Mkoa sasa hivi..” Hisham hakutaka kutoa maelezo kwenye simu kwani aliamin maswali yatakua mengi kuliko yeye anavyoweza kuyajibu..
“Sawa..ngoja nifanye hivyo” Alijibu Regina aliyekuwa Makorora kwa dadaake wa kwanza Rahel Madaba..
Ilimchukua takriiban dakika kumi tu alishakua hospitali ya mkoa. Akampigia simu Hisham ambaye alimuelekeza wapi pa kuwapata..
“Hivi wewe damu yako ni grup gani?” Hisham ambaye siku zote huwa hapendi kurefusha maelezo, alimuuliza Regina baada tu ya kuonana..
“O, mi ni grup O” Alijibu Regina kwa kujiamini na kumfanya bi Nana Amiry ambaye alikuwa amekaa kwenye bench pale nje akilia, kunyanyuka haraka na kuja kumkumbatia Regina na kutoa tabasamu zito kisha akatamka kwa nguvu..“Ooohh..Alhamdulillah..”
“Wahi haraka kwa daktari ukachangie damu tuna mgonjwa anahitaji damu ya grup O..” aliongea Hisham akimuelekeza na kumsindikiza Regina hadi chumba cha daktari..
*********
Hisham kabla hajarudi kukaa pale kwenye benchi alipokuwepo, simu yake iliita..akapokea..
“Kaka, nimekutumia e-mail mda sana naona hujajibu..unanipa wasiwasi..” Aliuliza Khatib baada ya kusubiri zaid ya dakika kumi sasa bila majibu kwa electronic mail(e-mail) aliyoituma kwa Hisham..
“Samahani kaka, daah ila Mungu mkubwa..amekuja mke wangu ndio yupo huko kwa daktari wanamtoa damu ili awekewe mgonjwa, wewe vipi Mama umewasiliana nae?”
“Yaah..kumbe wapo wote Tanga na na yule mdogo wangu Hawa..maana Hawa naye ni Group O..sasa mi niliwaambia utawapigia simu ili uwaelekeze waje hapo hospitali”
“Aaah wee waache tu usiwasumbue tena, waambie tayari msaada wa damu umepatikana kwahiyo waendelee na mambo yao tu hapa tumeshamaliza tatizo..” Hisham alimjibu Khatib kwa kujiamini, ambaye naye baada ya kuridhishwa na majibu ya Hisham alikata simu na kumpigia simu mamaake akimwambia kuwa tatizo tayari limeisha..
**************
“Ngoja tuangalie haya majibu vizuri kwanza kabla ya kuanza zoezi letu la kutoa damu” Dr Elisha aliyasema hayo huku akichukua karatasi moja nyeupe iliyotoka 'Lab' ambayo ililetwa pale chumba cha daktari na muuguzi mmoja wa kike aliyevalia sketi na shati na raba, vyote vikiwa vyeupe.
“Ok, nakusikiliza Dokta..” Regina alisema huku akijiweka vizuri katika kiti kile akijisogeza mbele.. Huku macho yote kwa Dokta Elisha..
Kisha kimya kikatawala huku Dr Elisha akiwa amekodolea macho ile karatasi haamini anachokiona..kisha akajikohoza kidogo pasipo kuonyesha tofauti yoyote kwa Regina..
“Regina, ni kweli wewe una damu ya grup O haswa..lakini damu yako haiwezi kufaa kuchangia mgonjwa wetu”
“Kwanini Dokta? Ina tatizo gani kwani?”
“Haina tatzo lolote, isipokuwa tu hai-match na mgonjwa wetu..”
“Mmh.. Dokta usinifanye mi mtoto bwanaa..niambie tu kama nimeathirika bwanaa...” Hapa Regina alijikaza kusema maneno haya huku akiwa anabishana na nafsi yake lisiwe jambo hilo kweli..
“Mara ya mwisho kupima HIV ilikuwa lini??”
“Siku nyingi sana Dokta, hata sikumbuki”
“Ukipata muda uje hata kesho tufanye vipimo zaidi kuhusu afya yako kisha nitakwambia kwanini damu yako hailandani na mgonjwa..ok?” Dokta Elisha alijaribu kukwepesha ukweli kwa sababu hayakuwa madhumuni ya Regina kuja kupima Ukimwi..hivyo majibu ya kuwa ameathirika hayakumstahili kwa muda huu..
Ingawa Regina mwenyewe alishapata picha halisi ya nini kinaendelea hapa baada ya maswali yale aliyokuwa akiulizwa na Dr Elisha..
Wakati Dr Elisha akitafakari kuhusu nini cha kufanya huku akiwa tayari ameshamruhusu Regina atoke chumba cha daktari.. Mlango wa kuingilia hapo chumbani kwa Dokta Elisha ukafunguliwa, akaingia muhudumu mmoja ambaye alionekana kuwa daktari msaidizi, aliingia kwa kasi huku akihema juu juu..
“Dokta, hujakamilisha bado zoezi la damu kwa ajili ya Abdul? Maana hali yake kwa sasa ni mbaya mno..” Aliuliza Muhudumu yule huku amemkodolea macho Dr Elisha ambaye alionekana kukosa majibu.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Let's call it a day..!!
Tusubiri Episode O15
www.mdharubajk.blogspot.com
Whatsapp↘
+250726023140
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni