Jumatano, 27 Mei 2015

HISTORIA BATILI O9

STORY: HISTORIA BATILI(Fake History)
MTUNZI: Jumaa Khatib Mdharuba (Jk)
+255 718 274 130
+255 756 274 130

EPISODE O9
★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Ila Mama, tunazika leo ndio, ila hiki kifo cha mdogo wangu mimi nina wasiwasi nacho sana.. Sidhani kama ugonjwa tulioambiwa ndio kweli aliokufa nao, nahisi kuna kitu zaidi ya hivyo” Alianza kuhoji bwana Kulwa Yassini-kaka mkubwa wa Sauda upande wa mamaake, wakiwa wamezaliwa mama mmoja lakini kila mtu na baba yake..akiwa anajaribu kumshauri mamaake kutokubaliana na Dokta Mwinyi..daktari bingwa wa magonjwa sugu, hasa yanayowahusu wanawake..
Kulwa Yassin alikua akiishi nchini Rwanda akifanya kazi kama afisa mikopo katika benki moja iliyopo katika Mtaa wa Kabuye Jijini Kigali..Alikua akiishi maisha mazuri sana, yeye ndiye aliyekua tegemeo pekee la mama yake..na aliitendea haki nafasi yake haswaa..Alimuenzi sana mama yake akiwa anamtumia pesa karibu kila baada ya wiki moja..
Kifo cha Sauda kilimshtua sana, aliharakisha sana ili awahi mazishi na kujua kiundani haswa nini sababu ya kifo hicho..
Wakati akijadili haya na mama yake watu walikua tayari wamekusanyika nyumbani kwao tayari kwa ajili ya mazishi yaliyopangwa kufanyika saa 10 jioni, na muda huo ilikua yapata saa 8:45 mchana..
“Mwanangu, mimi nimechanganyikiwa hapa, sielewi hata ni nini unachokiongea, naomba tuangalie haya ya mazishi kwanza halafu hizo hoja zako zingine utazileta baadae..” Aliongea mama Sauda machozi yakimbubujika usoni..
“Hapana mama, huu mwili ni lazima tukaufanyie uchunguzi katika hospitali nyingine, maana mazingira ya kifo cha mdogo wangu mimi siyaelewi..!!”. Kulwa aliona atoe yale ya moyoni, japo alijua fika kuwa muda umeenda sana na mwili wa marehemu ulishalala hospitali siku moja, na taratibu za waislam ni kuwahisha kuzika, hivyo kwa kuzikwa leo saa 10 tayari Sauda alikua amechelewa sana kuzikwa tangu alipofariki. Anapoleta wazo la kwenda kufanyia uchunguzi mwili wa marehemu anamaanisha anamsogezea zaidi siku za kuzikwa, na vilevile ni jambo gumu kwani watu wote walishakua na taarifa za mazishi kuwa yatafanyika leo saa 10.
Ila, Kulwa bado aliendelea kusisitiza kuwa alitaka kwenda kuufanyia mwili ule uchunguzi kwenye hospitali tofauti na Alhaj Hospital ili ajiridhishe na kifo cha mdogo wake..
Kama wasemavyo pesa ina nafasi kubwa katika maamuzi kwa maisha ya leo kuliko hata umri, Kulwa alishinda hoja yake na akakubaliwa aupeleke mwili kwa ajili ya uchunguzi kwenye hospitali nyingine.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
Wakati anaongea na mwanae Abdul, Mr Khatib alisikia beep tone katika simu yake ikiashiria kuna ujumbe mfupi (sms) imeingia katika simu yake..Akaitoa simu yake sikioni na kuweka 'loudspeaker' kisha akaanza kusoma ule ujumbe aliotumiwa..
Ndipo hapo alipojikuta akitoa sauti kubwa ya kushangaa.."Aaaaaaaaaghh" akawa ameduwaa hajui nini afanye. Akaiacha simu ikiwa bado hewani kwa dakika kadhaa kisha akaikata, na kurudia tena kuisoma ile sms iliyokua imetumwa katika simu yake na Hisham Omari Mikidadi iliyosomeka..
"Boss, Yule ---- Kulwa analazimisha auchukue mwili wa Sauda akaufanyie uchunguzi katika hospitali tofaut na Alhaj Hosptal, tunafanyaje hapo boss?”.
Khatib hakuwa anaamini hiki anachokisoma katika simu yake,ila haraka sana akaamua kuifoward ile sms kwa mama yake Mama Mdharuba ambaye naye alikuwepo pale msibani..
Baada ya takriiban dakika mbili simu yake ikaingia ujumbe mwingine kutoka kwa mama yake, “0726023140 piga hiyo namba halafu mwambie mimi ni mtoto wa Mama Mdharuba kisha umueleze hili jambo, fanya hivyo sasa hivi”.
Khatib hakuwepo eneo la msiba muda huu licha ya kuwa yeye ndiye Mume wa marehemu, ingawa hakuna aliyekuwa anahoji kwani kabla ya hapo alishakuja mara nyingi sana pale msibani akiwa anawajibika kwa kila jambo, kwahiyo 'kuchomoka' kwa dakika kadhaa pale msibani hakukuwashtua watu kwani walimjua vizuri Khatib kuwa ni mtu mwema tu hana tatizo haswa ukizingatia bado muda wa kuzika haukuwa umefika..
“Haloo, Khatib Mdharuba, mtoto wa Mama Mdharuba” aliongea Khatib baada ya simu yake kupokelewa..
“Oooh, mama yako amenitumia ujumbe tayari na amenambia kuwa utanitafuta..” Aliongea bwana yule ambaye alijulikana kwa jina la Sheikh Lesangwa kwa watu wote waliomfahamu.
“Sasaa..Khatib sheikh wangu huyo mzembe anataka kutafuta umaarufu kupitia jina lako, sasa usiwe na wasiwasi, hakuna atakachofanya, naomba uniamini na uniachie mimi hiyo kazi, ila nitakuomba ufanye kitu kimoja kwa sasa, nenda haraka sana hapo msibani na umpe mkono kwa kusalimiana nae, kabla hajatoka na marehemu, wahi” Aliongea sheikh Lesangwa ambaye alionekana kulijua vizuri jambo linavyoendlea. Haikuhitaji maswali mengi kwa bwana Khatib zaidi ya kuitikia “Sawa” na kukata simu, maelezo yalishajitosheleza.
Akatoka haraka sana na kuchukua gari yake aina ya Land Cruiser-Prado TX na kuelekea moja kwa moja msibani. Ndani ya dakika 5 tayari alishafika msibani kwani palikua si mbali na nyumbani kwake. Moja kwa moja hadi ndani ambapo alikutana na bwana Kulwa na kumuomba waje waongee mara moja..
Alitoka bwana Kulwa na wakasalimiana kwa kupeana mikono kisha mazungumzo yakaendelea..
“Nambie kaka, nilitoka kidogo hapa, vipi kuna chochote ambacho kinaenda tofauti? Maana na muda wenyewe umekaribia sana huu..” Aliongea Khatib akijifanya hajui chochote kuhusu uchunguzi wa mwili ambao Kulwa alipanga kwenda kuufanya.
“Yeah mabadiliko yapo, maana nipo katika maandalizi ya kwenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa mwili wa marehemu, sijaridhika bado na maelezo ya Dokta Mwinyi” Alifunguka bwana Kulwa.
“Oooh, oky sawaa.. Ila sasa shem kama umeamua kufanya hivyo ni vyema ukawaambia hawa watu waliokusanyika hapa nje mapema, maana hayo mazishi hayatakuwa ya leo tena” Alishauri Khatib, moyoni bado akiwa na wasiwasi mkubwa.. Kwanza hajui kwanini aliambiwa aje ampe mkono Kulwa, pia hajui kuwa huyo Sheikh Lesangwa ana kipi haswa cha kufanya katika hili ili hili tukio lisitokee..Kwa muda mfupi sana alishawaza mambo mengi mno huku akimuona bwana Kulwa akiwa anamaanisha alichokisema..
“Itakuaje endapo atauchunguza huu mwili na kugundua kifo chake kimetokana ma kuvuta sumu??” “Nani atakua wa kuulizwa kuhusu hiyo sumu zaidi ya mimi mumewe?” “Na nikigundulika kuwa nimempa sumu kwa njia ya hewa mke wangu, jamii itanichukuliaje?” Maswali yote hayo yalizunguka kichwani kwa Khatib, lakini hakuna hata moja liliokuwa na jibu wakati huo.
*******************************
“Mwanangu, hilo jambo unalotaka kufanya ni gumu sana, na utatafuta uhasama na watu, hivi unafikiri shemeji yako Khatib atakuchukuliaje?? Sauda ameshakufa, acha tu aende akapumzike kwa amani huko mwanangu, una lazima gani ya kufanya uchunguzi? Hivi wewe unafikiri una uchungu zaidi na Sauda kuliko mimi niliyemzaa mwenyewe? Hao watu hapo nje wote wanasubiri wakazike, sasa ni saa 9:15, bado nusu saa tu waende na mwili msikitini kwa ajili ya kuuswalia, hivi unawaambiaje mazishi yameahirishwa?? Mbna watoto wa siku hizi mnakua hivyo jamani??” Mama Sauda alilalama sana kumlalamikia mwanae ambaye alionekana amekua mbishi na analazimisha kufanya jambo gumu bila hata kuhofia chochote,..Ndio, hakuhofia kitu, na ndio kawaida ya pesa, ukiwa na pesa na uoga unaondoka, kinachoongezeka ni confidence tu!!.
“Mama mi acha tu nipate ukweli wa hiki kifo, wewe nione mkorofi au vyovyote tu, lakini mimi lazima nikachunguze kwa makini kifo cha Sau....” Kabla hajamalizia sentensi hii ghafla alishtuka akashikilia tumbo lake na kukimbilia chooni.
★★★★★★★★★★★★★★★★★★

Watch Out Episode 10

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni