Jumatano, 27 Mei 2015

HISTORIA BATILI O8

STORY: HISTORIA BATILI(Fake History)
MTUNZI: Jumaa Khatib Mdharuba (Jk)
+255 718 274 130
+250 726 023 140

EPISODE O8
★★★★★★★★★★★★★
"Kaka, nimepokea sms hapa kutoka kwa boss, hebu isome" Aliongea Hisham akimpa simu Haroun na kusoma ile sms ilotumwa na Mr Khatib kwenye simu ya Hisham..
“Duuuh..kaka, hatari.., sasa tunafanyaje hapa?” Haroun ambaye alionekana kuduwaa zaidi aliuliza..
“Tufanye kama alivyotuelekeza, vitu vingine tutajua baadae..” Aliongea Hisham na kuongozana na Haroun kuelekea maeneo ya Alhaj Hospital kuonana na Dokta Mwinyi Moh'd, daktari maarufu wa magonjwa sugu hasa kwa akina mama..
Dokta Mwinyi alimiliki hospitali yake mwenyewe licha ya kuwa alikua pia ameajiriwa katika hospital ya serikali..
Walifika, wakaongea nae kwa muda wa takriiban dakika 24 na kuonekana kukubaliana jambo.
Kisha baadae ikaonekana Ambulance ikiingia kwa kasi hospitalini hapo akishuka Mr Khatib na mgonjwa aliyekuwa kwenye machela akiongozwa na wahudumu wawili wa kike wote wakazama ndani hospitali.
******************************
“Dokta, nini hasa sababu ya kifo cha mwanangu??” aliuliza mama Sauda baada tu ya kufika hospitali na kuonana na Dokta Mwinyi ambaye ndiye haswa aliyehusika na mgonjwa yule. Dr Mwinyi alishatoa taarifa juu ya kifo cha Sauda.
“Kumbe wewe ndo mama Sauda, kwanza pole sana mama, usihuzunike sana licha ya kuwa nafahamu jinsi unavyojiskia kwa sasa, kifo hakikwepeki, kwahiyo yapaswa uushinde moyo wako ili uweze kukubaliana na ukweli kuwa Sauda ameshafariki na hakuna namna ya kuirudisha pumzi yake tena...” Aliongea Dr Mwinyi kisha akaweka pozi kabla ya kuendelea,...
“Naaa...kuhusu sababu ya kifo chake, ni kuwa Sauda alipata saratani ya shingo ya kizazi, ambao huu ni ugonjwa hatari sana, kwa hapa kwetu Tanzania kila mwaka wanawake zaidi ya 40,000 wanaambukizwa ugonjwa huo. Naaa..ugonjwa huu unasababishwa na virusi ambavyo kitaalamu vinajulikana kama Human Papilloma Virus (HPV). Tatizo kubwa ni kuwa ugonjwa huu hauna dalili za mwanzoni, mpaka mtu awe na kawaida ya kucheki afya yake mara kwa mara ndo atagundua, ila baadae dalili kuu mbili tu ndo huwa zinajitokeza ambazo ni uvimbe katika kinena na maumivu makali wakati wa kujamiiana, hizi ni dalili za mwishoni. Ilaaa..kwa mujibu wa maelezo ya Mr Khatib mwenyewe ni kuwa alikua hafanyi mapenzi na mke wake mara kwa mara, yaani alikua akikaa mda mrefu saana.. Hivyo ni ngumu kugundua dalili hii ya maumivu katika tendo, na dalili hii ya uvimbe katika kinena mara nyingi ni ngumu kugundua sababu wanawake wengi wanaona aibu kuongea tatizo hli kwa watu wao wa karibu.. Kwahyo mama, Sauda anaonekana aliugua huu ugonjwa kwa mda mrefu saana, lakin alikua HAJUI.., Pole sana, Mungu atawapa wepesi katika msiba huu mzito..” Alimaliza maelezo Dr Mwinyi na kumfanya Mama Sauda kukosa hata swali la kumuuliza..
Akanyanyuka na kushika kitasa cha mlango akaufungua na kutokomea..
★★★★★★★★★★★★★★★★★★
“Mama, kwa sasa nimeshakua mkubwa, nakuomba plzzz..niambie baba yangu ni nani!!”
“Mwanangu, kusema ukweli kutomjua babaako ni salama zaidi kuliko kumjua, mi namfahamu vizuri yule babaako, sio mtu mzuri kabsaa..licha ya kuwa machoni kwa watu anaonekana mwema”..
“Mama, mi nishakwambia kuwa ili uwe na amani na mimi kwa sasa ni kunionesha tu babaangu, nina miaka 9 sasa, kwanini bado tu unaniona mtoto?, mi namtaka babaangu” Aliendelea kusisitiza Abdul-mtoto wa darasa la 4, ndo kwnzaa akiwa na miaka 9, umahiri wa akili yake ndio ulifanya aandikishwe darasa la kwnza akiwa na miaka 6 badala ya 7, alikua ana akili ya ziada.. akilelewa na Mama yake bi Hamida Hassan aliyekua akimpenda sana mwanawe huyu wa pekee..
Alijitahidi kuhangaika sana kutafuta kuhakikisha mwanawe anaishi katika mazingira salama na anakua na furaha.
Baba wa mtoto, Mr Khatib, hakugombana na Hamida bali Hamida alijitenga nae baada tu ya kuzalishwa mtoto huyu sababu alihisi Mr Khatib atakua ana nyodo sana na anaweza kumnyanyasa na mtoti wake..
Hamida Hassan alikutana na Khatib miaka 11 iliyopita wakati Hamida alipoenda na wazazi wake kutembelea Hifadhi moja ya wanyama kijijini Kiwavu, Khatib akiwa kama ndio muongozaji mkuu wa eneo lile kwani alibahatika kusoma na kuelewa vizuri kuzungumza Kingereza pamoja na Kifaransa..
Hamida alimpenda sana Khatib na wakawa wakiwasiliana kutokea hapo mpka ambapo Hamida alipata mimba ya Abdul, wakiwasiliana vizuri mpaka mtoto alipozaliwa hadi alipofikia miaka miwili. Baada ya maisha ya Khatib kubadilika ndipo Hamida alipoamua kujitenga nae.
*******************************
“Haloo..”
“Yes, haloo”
“Habari za huko?”
“Nzuri tu, nani anaongea?”
“Mama Abdul”
“Ooooh Hamida, za siku tele mama watoto? Ukaaamua kunisusa, nimekutafta weee sijui uko wapi, vipi Abdul anaendleaje??” Aliropoka maneno mengi sana Mr Khatib baada ya kujua anaongea na Mama wa mtoto wake.
“Mi niko poa, mwanao huyu ongea nae” Alijibu kiufupi Hamida na kumkabidhi simu Abdul, hakutaka mazoea tena na Khatib, sababu zake alikua anazijua mwenyewe..
“Shikamoo dady..” Abdul alianza baada tu ya kupewa simu..
“Marahaba, hujambo mwanangu?”
“Sijambo, eti daddy wewe unaitwa Khatib nan?”
“Hahhaaahaa..mimi ni Khatib Mdharuba mwanangu..”
“Waoooh daddy i know you, wewe ndo yule tajiri kumbee.. ”
“Aaaaaaaghhhhh....” Ni sauti iliyotokea upande wa Baba Abdul na kumfanya Abdul ahamaki sana na kuanza kumuita babaake...
“Daddy..daddy..daddy....” Abdul aliita mara kadhaa bila ya majibu upande wa pili.. Hamida akachukua simu na kuiweka sikioni, bado ilikua haijakatwa lakini upande wa pili alikua haongei..
“Baba Abdul.., Baba Abdul..,,..iiishhhh...baba Abdul...Baba Abduliiiiiii...” Aliita mara nyingi Hamida lakini hakukua na majibu yoyote..
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Watch Out Episode O9

Maoni 1 :

  1. DR WALE on kindel, et see on 100% teie jaoks .. TEMA WHATSAPP +2347054019402
    Ma tahan tänada dr Wale'i, kes mu armastatu 72 tunni jooksul minu juurde tagasi viis. Kui mu väljavalitu mind maha jättis, olin nii väsinud ja pettunud, kuni otsisin internetist abi ja nägin dr Wale ofist (drwalespellhome@gmail.com) nii palju head juttu ning otsustasin proovida ja võtan temaga ühendust ning selgitan minu probleemid temaga ja ta pani mulle armastuse loitsu, mida kasutasin oma mehe tagasi saamiseks. Kui soovite oma väljavalitu tagasi saada, võtke WhatsAppi kaudu ühendust Dr. Wale'iga: +2347054019402 VÕI E-post: drwalespellhome@gmail.com

    JibuFuta