Jumatano, 27 Mei 2015

HISTORIA BATILI O6

STORY: Historia Batili
MTUNZI: Khatib Jumaa Mdharuba.
+255 718 274 130

SEASON O1-EPISODE O6
★★★★★★★★★★★★★★
Tukio la Alice kupigwa risasi ya kichwa lilimshangaza sana Noor sababu hakutegemea.. Alipigwa risasi kutoka katika bunduki iliyokuwa imewekwa kiwambo cha kuzuia sauti. Hivyo hawakuweza kusikia mlio wa risasi na hawakujua imetokea wapi..
Wakati bwana Noor amemuita Hisham wakiwa wameduwaa wakijishauri cha kufanya huku baadhi ya wateja wa Pub ile wakiwa wameshajua nini kinaendelea..Ghafla ikaingia gari ya polisi aina ya LandCruiser na kubeba mwili wa marehemu huku wakimchukua bwana Noor kwa mahojiano zaidi.
"Sheenzi kabisa, hawa Mbwa sijui wamepata wapi taarifa za haraka namna hii" Alilalama Bwana Hisham huku akielekea Ofisini kwake kujiandaa kuelekea kituo kidogo cha Polisi cha Msamvu ambapo ndipo Noor aliachwa pale na polisi wakaelekea katika hospital ya Mkoa Morogoro kwa ajili ya uchunguzi wa maiti ya Alice..
"Nani ndio mkuu wa zamu kati yenu??" Swali aliloanza nalo Hisham punde tu baada ya kufika kituon hpo na kukutana na askari watatu wa kituo kidogo cha Msamvu.
"Aisee hii mijitu mingine sijui ikoje jjamani, jitu rinakuja hapa rinakuta watu hata saramu harina.." Alilalama polisi mmoja na kuelekea ndani ya kituo kile na Hisham kufuatia nyuma..
"Wewe umekuja hapa kusalimiwa au kufanya kazi?? Kama unataka kusalimiwa tembelea Nursery huko au shule za msingi" Alibwabwaja Hisham akionesha ujeuri wake na yeye..Kikubwa kilichomshaua bwana Hisham ni pesa alizokuwa nazo katika biashara zake haramu walizokuwa wakishirikiana watu wawili, yeye na Manager wa Euler Hotel Mr.Haroun Rashid na kwa sasa wakiamua kumshirikisha Mr.Khatib kama mtu wa tatu ambaye alikua na urahisi wa kuzitoa cocaine na Heroine Canada na kuzivukisha boda bila wasiwasi mpaka Tanzania kwani alishasafirisha mizigo kwa muda mrefu sasa kati ya nchi hizi mbili hivyo alikua na urahisi katika kazi yake.
"Sema shida yako sasa nakusikiriza" Aliongea askari yule ndani ya kituo kile kidogo cha polisi..
"Nahitaji kumwekea dhamana Mr Noor A Mdharuba ambaye ameletwa hapa kituoni muda si mrefu" Hapa Hisham alionekana kuongea kwa busara kidogo.
"Huyu muuaji??" Aliuliza askari yule akimkodolea macho Hisham na kumfanya Hisham ahamaki..
"Muuaji?? kwani mmeshafanya uchunguzi na kubaini kuwa yeye ndiye aliyeua?"
"Hapana, ila yeye ameletwa hapa kwa kesi ya mauaji na tunahitaji kufanya mahojiano naye zaidi"
"Sasa wewe una mamlaka gani ya kumuita kuwa ni muuaji wakat hata mahojiano bado?? Au umechanganyikiwa??" Safari hii Hisham alishapanic..
"Mimi sijachanganyikiwa, ila huwezi kupata dhamana ya hyu mtu mpaka tufanye naye mahojiano kwnza"
"Fanyeni basi mahojiano mimi namsubiri hapa" Aliongea hivyo Hisham akidhani taratibu za kipolisi ni za rahisi kiasi hicho.
"Hapana, huyu ataandika maelezo kesho asubuhi halafu ndo tuangalie utaratibu wa dhamana, kwa leo atalala hapa" Alimalizia maelezo yule askari na kumuamuru Hisham atoke nje ya kituo kile..
Hisham akatoka na kuingia katika gari lake akiwa hajui nini cha kufanya..
Akaamua amtumie ujumbe Mr Khatib juu ya tukio lile.
Mara simu yake ikaita, akapokea na kuweka sikioni.
"Nafahamu kila kitu Hisham, rudi nyumbani kapumzike" Kisha simu ikakatwa, hiyo ilikua sauti ya Khatib akiongea akiwa nyumbani kwake.
Kisha akapiga simu ya mkononi ya mkuu wa kituo kidogo cha polisi pale Msamvu..
"Haloo Mkuu, kuna kijana anaitwa Noor yupo hapo kituoni kwako ndio ameletwa usiku huu, huyo ni wangu"
"Ok boss, nko nje ya kituo sina taarifa samahani sana" Alisema askari yule kisha akakata simu.
Simu kituoni ikaita na akapokea askari aliyekuwa mkuu wa zamu siku hiyo akaonekana kukubaliana kitu kisha akakata simu.
Akaelekea moja kwa moja katika chumba kimoja kidogo kilichokuwa na giza sana na mlango wa chuma, akafungua na kumruhusu Mr Noor atoke.
★★★★★★★★★★★★★★
Ilikuwa ni jumapili moja ambayo bi Sauda alikuwa nyumbani akifanya usafi na kujaribu kupanga panga vizuri vtu vya nyumbani baada ya kumaliza kufua kazi ambayo aliianza tangu saa 11 alfajiri na kuikamilsha saa 1 asbuhi. Licha ya kuwa ofisi yao ilifunguliwa pia siku za Jumapili na kufungwa mapema, lakini Jumapili hii Sauda aliamua amuachie majukumu yote Nira ili aweze kusimamia maendeleo ya pale sehemu yeye akifanya majukumu haya ya nyumbani siku ya leo.
Akaamua kuzitoa nguo zote kabatini ili azipange upya. Akaanza na za kwake ambazo alizitoa zote na kuzikung'uta vumbi na pia akafuta vumbi pale kabatini kisha akazikunja upya na kuzirudisha kabatini katika mpangilio mpya!!.
Akahamia upande wa nguo za mumewe na kuzitoa zote na kuzitupia kitandani na ili azikunje upya. Ndipo alipohisi kama kuna ktu kimeanguka kutoka katika zile nguo alizozitoa pale kabatini. Akajaribu kuangalia vizuri pale chini akaona kitu kama kitabu kidogo hivi cha kijani. Akakishika na kuangalia vizuri akagundua kuwa ni pasi ya kusafiria. Akaweka pembeni kisha akaendelea na zoezi lake la upangaji nguo.
Alipomaliza akachukua ile pasi ya kusafiria na kutaka kuirudisha mle kabatini, lakini kabla ya kuirudisha akaamua kuifungua na kuikagua mle ndani.
Akaipitia kwa makini sana na kujikuta akihamaki kwa nguvu..Laahaaaulaaa!! Akiweka mkono wake mdomoni huku mdomo ukiendelea kubaki wazi akiwa haamini anachokiona hapa!!
Pasi hii ilionesha kuwa muhusika alionekana kusafiri kutoka Tanzania kwenda Canada na baadaye kutoka Canada hadi Norway wiki 5 zilizopita.. Akajaribu kukumbuka kilichotokea, akanyong'onyea.
Wakati bado anaendelea kutafakari huku akiichunguza vzuri hii pasi, akagundua kitu kingine ambacho kilimstua zaidi.
Pasi ilikua na picha ya mumewe-Khatib, lakini majina yaliyokuwepo katika pasi ile ni Mwatete Mwandaro Mwinjuma!! Akazidi kuduwaa mara hii akiegemea kioo cha kabati lile taratiib akielekea kukaa kitako sakafuni huku macho kodo katika 'Passport' ile.
Wakati yupo hapa chini amekaa kitako, likaja wazo moja kichwan kwke ambalo aliamua kulifanyia kazi..
Akanyanyuka kutoka pale chini na kurudi pale juu kabatini kisha akatoa nguo zote za Khatib akazitupa kitandani na kuanza kufanya 'search' ya maana..
Alikutana na vitu viwili vingine ambavyo vilizidi kumuumiza kichwa..
Kwanza, alikutana na kitambulisho cha kupigia kura ambacho kilikuwa na picha ya mumewe na jina lile la Mwatete Mwandaro Mwinjuma kitambulisho kilichotolewa katika kijiji cha Kiwavu Kata ya Tongoni, Wilaya ya Tanga mjini, Mkoani Tanga miaka 8 iliyopita.
Pili, alikutana na Cheti cha kuzaliwa kikiandikwa Jina mtoto kuwa ni Mwatete na jina la baba kuwa ni Mwandaro Mwinjuma, cheti kikionesha mtoto amezaliwa Hospitali ya Mkoa ya Bombo Mkoani Tanga tarehe 14/10/1987. Hapa aliduwaa zaidi maana hii ndio tarehe aliyozaliwa mumewe.
"Mwatete?? Mmmmh..na hii Khatib imekujaje? Mbona sielewi hapa?" Alijiuliza moyoni bi Sauda baada ya kujiridhisha kuwa hivi vitambulisho vyote ni vya mumewe.
★★★★★★★★★★★★★★
Don't Miss Episode O7.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni