Jumanne, 26 Mei 2015

HISTORIA BATILI O5

STORY: HISTORIA BATILI-Fake History
MTUNZI: JUMAA KHATIB MDHARUBA(JK)
+255 718 274 130

SEASON O1-EPISODE O5
★★★★★★★★★★★★★★
"Haloo, kama zali yani, Khatib amenipa pesa na kunambia tukutane Mambo pub saa 3 usiku wa leo.." Ni sauti ya Alice katika sikio la bwana Ahmed Khamis Hamad.
"Mwanzo mzuri huo" Aliongea Ahmed na kuongeza.."Nenda nipo nyuma yako" kisha akakata simu.
Ahmed Khamis alikua kijana mmoja shupavu aliyekuwa anafundisha Somo la Stadi za kazi katika shule ya Msingi Mazimbu na pia alikua ndio Mwalimu wa Michezo katika shule hii.
Ila Ahmed alikua akifanya kazi pia kama Afisa usalama wa serikali ya Tanzania. Aliifanya kazi hii kwa miaka saba sasa lakini hakuna aliyekuwa anatambua hilo.
Baada ya kukabidhiwa jukumu la kufuatilia juu ya utajiri wa Mr.Khatib, ndipo alipokutana na Alice na njia pekee ya kumrubuni Alice ilikua ni kumtongoza awe mpenzi wke ili aweze kumtumia vizuri katika harakati zake.
Alishampa HISTORIA BATILI Alice kuhusu yeye(Ahmed) na Khatib na kudai kuwa Khatib aliwahi kutumia pesa zake nyingi kumrubuni mkewe mpaka wakafikia hatua ya kuachana. Kwahy kwa sasa alitaka kujua undani wake ili amchongee polisi aje amkamatishe katika mikono ya dola. Alice, kwa sababu ya uaminifu aliokuwa akionyeshwa na Ahmed na jinsi alivyokuwa akipewa pesa kila alipohitaji na saa zngne hta kabla hajaomba, alijikuta akimpenda sana mwalimu yule wa michezo. Akawa anafanya vile ambavyo Ahmed alimtuma kufanya.
Alice alikua akifanya mambo kwa upande mmoja akiwa hajui kuwa alikua akitumika vibaya. Upofu wake katika kupenda ulimfanya awe ----- sana na hakuwa hata na muda wa kufikiria katika alichoambiwa. Mwenzie Ahmed alishajua kuwa Khatib ni mtu hatari na anaweza kufanya chochote, kwahyo Alice akishindwa kumsaidia kufanikisha kazi angetafuta mtu mwengine ambaye angemtumia kama msaada. Hata kama Alice angeuawa hilo si jambo geni kwake, alishazoea..
********************
Alice alifika pale Mambo pub majira ya saa 2:56 usiku na moja kwa moja akatafuta meza ambayo ilikua haina mtu akafika na kukaa kwenye kimoja kati ya viti vilivyoizunguka meza ile.
"Unatumia kinywaji gani?" Swali lililotoka kwa mmoja kati ya wahudum wa pub ile..
"Naomba Kuku nusu"
Akakaa pale kwa muda wa dakika 6 na kushika simu yake na kuanza kupiga namba za Khatib. Simu haikupokelewa na badala yake ilikatwa kisha meseji ikaingia ikisomeka "Am driving, on my way to Mambo Pub, plz wait for me..i'll be there within 15 minutes" . Baada ya kusoma msg hii akaifoward kwa Ahmed kisha akaweka simu katika pochi yake ndogo na kuendlea kugonga kuku wake bila hata woga.
"Naweza kukupa kampani,? naona upo peke yako" Aliulza bwana Noor baada ya kufika katika meza ya bi Alice huku akimuangalia vizuri usoni kuhakikisha"
"Mmmh...aaaah.. kuna mtu namsubiria bado hajafika, unaweza kunipa kampani mpka atakapokuja" Alijibu Alice, tatizo lake kubwa Alice alikua hajui kukataa hasa pale anapoona dalili za pesa.
"Ok, asante sana.."
Alikaa pale bwana Noor na kuanza story za hapa na pale na bi Alice.
"Umesema unamsubiri nani vilee maana nshasahau eti mara moja hii.." Noor aliuliza swali la kimtego akijidai kama vile aliyetajiwa jina mwanzoni..hapa alikua anatafta pa kuanzia..
"Yaani nina promise na Mr.Khatib yule wa Saukhat Investment Company.. si unamjua??" Aliingia mzima mzima Alice pale alipokusudiwa kufika.. akiwa hajui kuwa maongezi haya yanasikika moja kwa moja katika sikio la Khatib kupitia earphone alizovaa akiwa kitandani na mkewe.
"Nasikia yule bwana ana pesa vibaya sana ila watu hawajui anafanya biashara gani haswa" Alianza kuchochea Noor.
"Yule ni balaa..kama sio unga sijuuii.. , maana nina waswas ile Euler hotel pia anamiliki yeye" Alijiachia Alice akiwa hana hili wala lile.
"Labda alirithi mali nyingi sana, maana nasikia babaake alikua tajiri mkubwa sana halafu alizaa watoto wawili tu" Noor Alijaribu kuigusia fake history kuangalia Alice anaichukuliaje..
"Sidhani, hata kama ni hivyo itakua bdo ana kitu cha ziada yule..Unajua kwanin nakwambia hvyo?? Yule anaweza akapotea hata mwezi nasikia hajulikani yuko wapi? Afu mbaya zaid hadi mkewe hajui..Naskia anapata tabu kweli mtoto wa watu anatafta mpka anakoma" Maelezo haya ya Alice yalianza kumpa picha flani Noor..lakin bdo akaendelea kuchimba zaid..
"Kwahyo unataka kunambia hyu mtu anaweza kuwa ni mafia?"
"Inawezekna maana nasikia pia ni mbabe, akitaka lake ndo hilo hlo..kwa mfano mi yule boyfriend wangu alishamgombanisha na mkewe..halafu baadae yule mwanamke alimtumia watu wamuue.." Maneno haya ya Alice yakampa picha Noor kuwa huyu Alice yupo nyuma ya mtu flani..Sababu Historia hii anayompa sasa ni ya kutunga-FAKE HISTORY. Mpaka hapa hakukuwa na sababu ya kumuacha Alice mzima, ingawa alitakiwa kufanikisha kumjua nani hyo yuko nyuma ya Alice..
"Yaaah nshawahi kusikia kitu kama hicho, ila huyo jamaa tu ndo simjui..na nasikia yupo Morogoro hii hii.." Noor aliongea kwa kujiamini na kuonyesha kuwa si mgeni na hizi habari ili apate kujua undani wa habari hii..wkati huu Noor alishamnunulia Alice pombe kali na kujikuta ameshasahau pia kuwa alikuja pale kwa madhumuni yapi.!!
"Boyfriend wangu ni mwalimu wa Michezo shule ya Msingi...." Kabla hajamalizia sentensi hii Alice alianguka pale alipokuwa amekaa huku damu nyingi zikimtoka kichwani..
★★★★★★★★★★★★★★
Mama Mdharuba, alianza kutilia mashaka juu ya mwanae Khatib kuhusu mambo anayoyafanya hivi karibuni. Na kabla mambo hayajawa mabaya aliamua kumuita mwanawe na kumpa onyo.
Pamoja na ubabe wke wote, Khatib hakuwahi kumdanganya mama yake kitu chochote..hivyo alipouliza kitu chochote na mama yake alikua hana option zaid ya kuongea ukweli!!.
Jumapili hii aliamua kuja kumuuliza maswali mawili matatu yahusuyo maisha yake kwa ujumla na mwenendo wke wa sasa.
"Nasikia sasa hivi umeanza kujiingiza katika biashara haramu mwanangu, ni kweli?" Aliuliza Mama Mdharuba wkat wako mezani wakipata chakula cha mchana..wakiwa na mdogo wake Khatib, Hawa ambaye alikua akiishi na mama yake katika jumba lile kubwa lililopo maeneo ya Mbezi.
Khatib alikaa kimya kana kwamba hajasikia swali hili..
"Siku zote nimekuwa nikikwmbia kuwa mimi sipendi niongee halafu ukae kimya..Naomba unijibu, unafanya biashara haramu au hufanyi?" Mama Mdharuba alianza kufoka.
"Mama nisikilize, hizo biashara sio zangu, ni za watu, mimi sina hata fungu katika hizo biashara mama!" Alijaribu kujitetea Mr.Khatib huku mamaake akimsikilza kwa makini.
"Siku zote nakwambi kuwa sitaki ushirikiane na watu wanaofanya biashara za haramu, sipendi na sitaki!! Kwanini hunisikilizi?? Mali zote hizo ulizokuwa nazo unatafuta nini tena mwanangu??"
Hapa Khatib alikuwa kama aliyemwagiwa maji ya baridi.
"Sasa ni hivii..ukirudi tena hapa nisikie umeacha hizo biashara zako za kipuuzi, la sivyo mimi na mwanangu tutakuachia nyumba yako turudi kuleee tulipotoka, nadhani unapakumbuka vizuri".Aliweka kituo kikubwa Mama Mdharuba na kumfanya Khatib azidi kutahayari.
"No mama plz usiseme hvyo.."
"Nasema hivyo sababu ya ujinga wako, mtoto mdogo namna hyo hata miaka 30 hujatimiza umekua na tamaa ya pesa kiasi hicho mpka unafanya biashara haram?? Sasa mi ntakukimbia..nakwambia hivyo.."
"Nimekuelewa mama, ntaachana nayo".
"Huyo mwenzio wa Canada ndo alokushawishi mfanye hiyo biashara??" Aliuliza swali la kizushi mama Mdharuba.
"Hapna mama, yeye hata hajui"
"Sasa ni nani mwengne mwenye uwezo wa kukushawishi?? kumbe wewe umekua mpuuzi siku hizi eeh?? Pumbaaavu" Alipatwa na hasira mama Mdharuba na kumzaba Khatib kibao cha shavu la kushoto.
★★★★★★★★★★★
Watch out epsode 06

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni