Ijumaa, 5 Juni 2015

HISTORIA BATILI O20

IRIWAYA: HISTORIA BATILI(Fake History)
MTUNZI & MWANDISHI: Jumaa Khatib Mdharuba
+255718274130

         EPISODE 20
★★★★★★★★★★★★★★★
Ilipoishiaa..
Hisham amekusudia kwenda kupima na Regina ifikapo kesho asubuhi..
Licha ya Nana kukataa mwanae asiende kuonana na Khatib lakini kupitia Sheikh Lesangwa, Khatib anafanikiwa kuteka hisia za Hamida na anaomba kuonana nae..

SASA ENDELEA...
Saa 2:00 asubuhi, Regina alishajiandaa kwa safari ambayo hakupewa maelezo ya kutosha na Hisham..
“Lakini si unambie kuwa tunaenda wapi mume wangu?”
“Wewe twende tu, utajua huko mbelembele..”
Wakatoka, moja kwa moja Hisham akaendesha gari lake hadi kwenye maabara aliyopewa majibu ya mwanzo kabisa, Jk Laboratory, Mazimbu..
“Sasa mke wangu, lengo la kukuleta hapa ni kuja kuangalia afya zetu, kwahiyo tushuke kwenye gari tukapate vipimo ili tujue afya zetu zimekaaaje” Hisham alisema wakiwa nje ya geti la maabara ile ambapo kulikuwa na parking kubwa tu.
“Sawa, hakuna shida mume wangu, your wish is my command..” Regina alijibu kwa kujiamini.
Wakaingia moja kwa moja ndani ya maabara ile na kukuta foleni ndogo ya watu wapatao watano, wakajiweka pale na kusubiri zamu yao.
“Yaani mume wangu wewe saa zingine una mambo ya ajabu jamaaniii..” Regina alianzisha mazungumzo wakiwa katika foleni ile..
“Kwanini unasema hivyo?” Hisham aliuliza huku akigeuza shingo kumwangalia Regina usoni.
“Sasa si ungeniambia tu kuwa tunakuja kupima mume wangu? Kwani mi ningefanyaje? Yaani mi nikajua sijui tunaenda safari ya wapi huko!” Regina alikuwa akisema maneno haya kwa kujiamini sana pasipo kujua kwenye akili ya Hisham kuna nini!  Alichokua anakiwaza Hisham hapa ni namna gani atamfukuza Regina nyumbani kwake baada ya majibu.
“Suprises are better than Promises” Hisham aliamua kujibu maelezo marefu ya Regina kwa msemo wa kingereza.
Walikaa pale takriibani dakika 24 mpaka zamu yao ilipofikia na wangaingia chumba cha Daktari pamoja. Hisham ambaye jana yake alipoondoka aliahidi kurudi na mkewe kwa ajili ya vipimo kwa pamoja, hakuwa na maelezo mengi kwa Dokta, ambaye alielewa tu kuwa Hisham aliamua kutekeleza alichoahidi.
★★★★★★★★★★★★★★★★
“Umefika?” Hamida aliendelea kupiga simu kila baada ya dakika kadhaa kuulizia kama Khatib amefika ama laa ili aweze kuonana nae. Tayari alishatoka nyumbani na kwenda katika hotel moja nzuri ambayo Khatib alimuelekeza amsubiri hapo. Baada ya dakika 20 tangu Hamida apige simu ya mwisho, Khatib alifika katika hotel ile maarufu jijini Tanga. Kutokana na umaarufu wake, Khatib alizama mpaka ndani kabisa kwenye kona moja iliyojificha ili isiwe rahisi kwa mapaparazi kufuatilia nini anafanya hapa. Akakaa na Hamida katika chemba hii na makusudio ya kikao hiki cha dharura yakaanza kutekelezwa.
“Kwanza, nafurahi sana kwa kukubali mwaliko wangu hapa leo, nakushukuru sana” Khatib alianza kuongea wakati muhudumu aliyeleta vinywaji kwa ajili yao akiwa ameondoka.
“Mimi pia nashukuru sana maana mama yeye alikua hataki kabisa tuonane lakini nimemtoroka” Hamida, ambaye wakati huu alishaanza kumuona mamaake kuwa hana maana alikuwa akifunguka tu, hakuwa anajua kuwa kuna nguvu ya ziada iliyotumika kumleta yeye pale.
“Na kwanini haswa mamaako alikua hataki tuonane wakati anafahamu fika kuwa sisi ni Wazazi?”
“Mimi hata sielewi, namuona ana roho mbaya tu, sasa mimi nisionane na wewe baba Abdul nitaonana na nani?”
“Ok, tuachane na hayo, nimekuja hapa tuzungumze kuhusu maisha yetu mke wangu.. Mimi nataka nikamilishe hatua zote za uchumba kisha tufunge ndoa ili tuishi pamoja”  Khatib aligonga moja kwa moja katika 'point' kitu ambacho ndicho kilichomleta hapo.
“Sawa..mimi nakusikiliza wewe tu” Hamida alijikuta hana cha kuongea, alishasahaulishwa kila kitu kuhusu yaliyotokea huko nyuma na Khatib, alishasahaulishwa pia kuhusu Dokta Idd..akili yake yote ilihamishiwa kwa Khatib. Kitu pekee alichokua anafanya yeye ni kuitikia tu kile alichotaka Khatib, kiwe sahihi au si sahihi.!! Ukiwa mtu maarufu na tajiri unakuwa na silaha nyingi sana. Na ni lazima uwe hivi hata kama hutaki, kwa sababu jambo la mtu masikini tu asiyejulikana huwa halionwi na macho ya wengi, kwahiyo hata ukifeli katika jambo fulani, watakaokuwa wanafahamu ni watu wachache sana na wala haliwezi kukuathiri kitu. Lakini kwa mtu tajiri na maarufu kufeli kwake ndio chanzo cha kuuzwa kwa magazeti, kuzungumzwa sana redioni na kwenye televisheni..na hata mazungumzo ya vijiwe vyote yanakua yanakuhusu. Na ndio sababu watu hawa hutafuta njia za kila namna kuhakikisha wanalinda 'status' zao zisije kushuka.. Kila nyanja ambayo itakua na msaada kwake, ni lazima aitumie ipasavyo. Khatib ni mmoja kati ya watu hao, na yeye ili kuilinda vizuri 'status' yake, alikuwa hajitokezi yeye hadharani kushughulika na matatizo yake, sehemu zote alikua akitumia watu, mamaake akimpanga sehemu nyeti kama hii ambayo haikuwa inahitaji usaliti kwa namna yoyote ile..
Noor yeye alikua akishughulika na mambo ya serikali, wakati Hisham yeye 'alideal' na 'rumours' zote za mjini. Haroun, ambaye kwa harakaharaka alionekana kama hana kazi kubwa, lakini naye alikuwa mtu muhimu sana kwani alikua akisimamia hotel kubwa sana 'Euler Hotel' huku akiwa ndio 'organizer' wa miradi yote mipya ambayo Khatib alikua akitaka kuanzisha.
Nira nae alikuwa mtu muhimu mno kwani yeye ndiye alikua akimuwakilisha Khatib katika matukio ambayo yalimuhitajia ila alishindwa kuhudhuria. Hivi ndivyo mgawanyo wa kazi ulivyokua na kila mtu alicheza sehemu yake vizuri na kwa mafanikio makubwa.. Watu hawa wote hawakua na mishahara kwa Khatib ila walikuwa na 'Allowances' zinazoendana na mapato ya kampuni. Hivyo majukumu yao waliyatimiza vizuri kwani 'income' yao ilitegemea zaidi mapato. Walikua hawana budi zaidi ya kujituma. Licha ya kuwa haikuwa mishahara, lakini walikuwa wanapewa pesa nyingi sana..kiasi cha kuwa hawakua na tamaa wala nia tu ya kusaliti.
Khatib aliongea mengi sana na Hamida pale hotelini, mpaka baadae ambapo waliamua 'kuagana' kwa 'kukumbushia enzi' katika moja ya vyumba vizuri vya hoteli ile.. Kisha Hamida akarudi nyumbani akiwa na milioni 1.3 ikiwa ni pesa ya 'matumizi madogo ya siku mbili tatu' kama alivyooita Khatib mwenyewe.
“Kazi imeisha mama, hapa kabaki Nana tu, yule mamaake” Khatib alipiga simu kwa mamaake kabla ya kuwasha gari kurudi Morogoro.
“Kama umemaliza kwa Hamida basi tu, mamaake hana shida yule, cha msingi ni Hamida mwenyewe tu”
“Ok, na yale maneno uliyonitumia kwenye sms nilitakiwa kuyasema kabla au baada ya tendo?”
“Kabla ya tendo mwanangu, au wewe umeyasema baada?”
“Hapana mama, nimesema kabla, nilidhani ni kinyume chake”
“Ooh, oky..kama kweli uliweza kupata nae tendo basi kazi imeisha mwanangu..Nana yule akimuona tu mwanae akili yake itahama, wala usijali.”
“Ok mama, ngoja niwahi kurudi nyumbani, nimechoka sana..”
“Ok, ila kama hujaoga rudi ukaoge, usiendeshe gari ukiwa hujaoga ni hatari sana”
“Hahhahaaa..mama bana, nilioga baada tu ya kumaliza mamaangu”
“Ok sawa, safari njema”
“Ok, ahsante sana”
★★★★★★★★★★★★★★★★
“Nyinyi ni wanandoa?” Dokta aliuliza kabla ya kutoa majibu, akiwaangalia Hisham na Regina usoni.
“Ndio, sisi ni wanandoa Dokta”  Hisham hakupoteza muda alitoa jibu la haraka.
Baada ya hapo daktari akaanza kuwauliza watakubaliana vipi na majibu yao, huku akijaribu pia kuwasihi wakubaliane na majibu yoyote yatakavyokua.. Akaongea mengi pia kuhusu kuwasihi waendelee kupendana na kushirikiana kama zamani endapo mmoja wao atambiwa ameathirika. Maneno haya ndiyo yalifanya Hisham ajue majibu kabla hata hayajatolewa.. Moyoni mwake akijisemea kuwa leo ndio mwisho wa Regina.
“Baada ya maelezo haya marefu, sasa naomba kuwapa majibu yenu, nikianzia na bwana Hisham hapo..damu yako ni safi kabisa (HIV negative), Hongera sana na endelea kuchukua tahadhari katika vishawishi na tamaa za kila siku, ngono zembe ni hatari sana.”
Kisha Dokta akageuka kwa bi Regina na kumuangalia..Regina ambaye alitabasamu akijua kuwa majibu yake yatakuwa sawa tu na Hisham..
“Kwa upande wako bi Regina, damu yako inaonekana imeathirika na virusi vya ukimwi(HIV positive). Ingawa huu sio mwisho wa maisha, bado una nafasi ya kuishi miaka mingi zaidi ukifuata utaratibu kama nilivyowaambia kabla.
“Dokta, you can't be serious?” Aliuliza Regina ambaye alionekana kushtushwa sana na habari ile. Akaanza kulia.
Tofauti pia na matarajio yake, Hisham alianza kumbembeleza na kumfariji, alishangaa sana, kitendo kilichomfanya anyamaze haraka. Kisha Hisham akamuaga Daktari na kisha akamshika mkewe mkono na kuondoka naye pale Hospitalini kuelekea nyumbani. Walipofika moja kwa moja wakaelekea chumbani kwao. Kisha Hisham akamuacha Regina pale na kuelekea sebuleni ambapo alibofya simu yake kumpigia Khatib.
“Kaka, huyu kahaba wangu hapa kakutwa na virusi, sijui nifanyeje?”
“Usikurupuke, as I did, then tutatengeneza sababu ya kifo”
“Ok kaka, nimekupata”
Mazungumzo mafupi yaliyoeleweka, yakamfanya Hisham akate simu, na kurudi chumbani kuendelea kimfariji mkewe.
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Let's call it A day..

Tukutane Episode 21👉 soon..

Follow IG: jk.stories

Sms/call: +255718274130

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni