Alhamisi, 14 Mei 2015

WALE WAPENZI WA STORY, TUANZE NA HII..HISTORIA BATILI

STORY: HISTORIA BATILI(Fake History)
MTUNZI: Jumaa Khatib Mdharuba (Jk)
+255 718 274 130

SEASON 01-EPISODE 01
★★★★★★★★★★★★★★★
"Mume wangu, huendi kazini leo??" Aliongea Sauda Ally ikiwa ni
Majira ya saa 3:30 asubuhi, hii ilikua sio kawaida ya bwana
Khatib Jumaa kuwa ndani mpaka muda ule.
"Leo sitoki" alijibu kifupi akiwa bado yupo kitandani akiwa busy
na simu yake..
"Ok sawa, mi nipo uani nafua kidogo".
"sawa". Alijibu bwana Khatib na kuendelea na ubize wake..
"Haloo Nira Saire..mimi leo sitokuja kazini kabsaa..naomba
muendlee na kazi kesho mtanipa ripoti kamili." alisema maneno
hayo baada ya simu kupokelewa upande wa pili.
★★★★★★★★★★★★★
Jumaa Khatib Mdharuba, kama alivyofahamika, alikua akijulikana
kama kijana aliyekulia katika maisha ya kitajiri sana, mtu ambaye
hakuwahi kuonja ladha ya shida katika maisha yake. Kipindi hiki
akiwa na umri wa miaka 27 tu alikua akimiliki yard kubwa sana
ya magari iliyokuwepo mkoani Morogoro. Alikua akifanya kazi
yake kwa ufanisi mkubwa kiasi cha kuwa na wateja wengi wa
uhakika kuliko hata wale washindani wake ambao walimiliki yard
hizo katika majiji makubwa kama Dar, Arusha, Tanga na
Mwanza. Aliuza magari yake kwa bei nafuu na yalikua na
warranty ya zaidi ya miaka mitatu. Alimudu kufanya kazi yake
vizuri sana, akawa anaishi maisha safi sana. Mpaka sasa
alishaweza kutoa ajira kwa vijana 15 ambao walikua wakishiriki
ktika shughuli tofaut katika yard ile, wakiongozwa na Nira Saire
kama kiongozi msimamizi wa wafanyakazi wa pale. Nira Saire
alikua akimuheshimu sana bwana Khatib kwa sababu alikua
akiishi nae vizuri na vilevile yeye ndiye aliyekua analipwa
mshahara mkubwa zaidi kuliko wafanyakazi wote wa pale. Mara
zote Khatib asipokuwepo majukumu ya kusimamia yalibaki kwa
Nira.
Nira alijaribu kutengeneza urafiki wa karibu saana na Khatib nje
ya kazi, lakini jambo hili linaonekana Khatib hakulipenda saana..
yeye alitaka awe anashirikiana nae zaidi kwenye kazi tu na
kutoruhusu saana wazoeane nje ya mazingira ya kazi..Nira
alilishtukia hili na akaamua awe mpole tu, kwanza aliamini watu
wenye pesa walikuwa na dharau sana..
Sauda Ally, mke wa Khatib, alijitahidi sana kuweka mapenzi ya
dhati kwa mumewe ambaye alikua na miaka miwili sasa kwenye
ndoa, ingawa Khatib hakuonekana kujali sana. Alikua busy sana
na mambo yake na mara nyingi akirudi nyumbani alikua
akipanda kitandani na kulala..hakuwa na muda wa kupiga story
na mkewe wala kuongelea maisha yao yanaendaje..
Wed, May 13, 2015 at 05:31Matendo yake yalikua yakishangaza watu wengi saana, na kila
mmoja alikua akimtafsiri tofauti. Alijitolea sana kusaidia masikini
na yatima na walemavu ila hakutaka chombo chochote cha
habari kihusike katika misaada hiyo. Alikua akitoa misaada
kimyakimya na akitembelea kituo kimoja anatoa zaidi ya mil.50!!
Alifanya hivyo kwa zaidi ya miaka mitano sasa..
★★★★★★★★★★★★★
Maelezo ya utajiri wa Khatib na mambo anayoyafanya
yalishangaza watu wengi sana..hakua na dharau wala kiburi kwa
mtu yeyote, ila swali kubwa lililokuwa akilini mwa watu wengi ni
kuwa "Kwanini anafanya kwa siri sana?"
Mambo yake aliyaendesha kwa siri kubwa,licha ya kumiliki yard
ya magari lakin tathmini ya utajiri wake ni zaidi ya hapa.!! hela
zingine anatoa wapii?? Na watu wote walijua kuwa alikua
akitokea katika familia ya kitajiri akimtambulisha Noor A
Mdharuba kama baba yake mdogo na mlezi wake anayeishi naye
hapa Tanzania wakati babayake mzazi alkua akiishi nchini
Canada akiwa ni Manager wa benk moja ya biashara nchini
humo.. Mara nyingi Khatib alikua akisafiri kwenda Canada
kuonana na baba yke Mzazi Mzee Jumaa Mdharuba.
Ni Noor ndiye aliyemshawishi Khatib kuoa mapema ili awe na
familia yake.
"Ila mimi sina hata mwanamke kwa sasa, ntamuoa nani?" Alihoji
bwana Khatib kipindi hcho..
"Kazi ndogo mwanangu, hiyo kazi ntamwachia Bi Nuro Ahmed
aniangalizie nani anaweza kuwa mke wa kuolewa na wewe.."
Alipangua hoja bwana Noor na kumfanya Khatib akubaliane nae..
Bi Nuro Ahmed ambaye alikua ni mmiliki wa kituo kikubwa cha
malezi na shule kwa watoto wadogo, alikuwa na wafanyakazi
wote wa kike katika kituo kile. Hivyo alikuwa akiwafaham vizuri
tabia zao na misimamo yao katika maisha. Aliweza kufanikisha
zoezi na kufanya bwana Khatib amuoe Sauda Ally ambaye Nuro
ndiye aliyempendekeza.
★★★★★★★★★★★★★★
"Mama, Khatib yupo huko kwako?" Alikua ni Sauda akiongea
baada ya salamu kumuulizia Mama yake Mzazi Khatib ambaye
alikua akiishi Mbezi jijini Dar..
"Hapana mwanangu, kwani vipi hajakuaga alipotoka?"
"Aliniaga kuwa anaenda kazini, lakini sio kawaida yke kutorudi
mpaka sasa.."
"Ucjali mwanangu, si wajua wanaume tena wanakutana na mengi
sana katika kutafuta" Mama Mdharuba Alijaribu kumliwaza mkwe
wake licha ya kuwa hakujua Sauda alikua anajickiaje..
Kwa miaka miwili aliyoishi nae alishamfaham vizur Khatib ni mtu
wa aina gani, mwanzo ilikua ngumu lakin baadae alizoea tabia ya
Khatib kutoka na baadae kupiga simu kuwa yupo sehemu tofaut
na aliyoaga.. lakini leo ni tofaut, haijawahi kutokea akatoka na
kuchelewa kurudi kias kile na mbaya zaidi simu yake haipatikani!!
Sauda alijawa na wasiwasi sana na kupiga simu sehemu zote
ambazo mumewe angeweza kupatikana.. lakini
hakufanikiwa..chakula cha jioni pia kilimshinda kula..sasa ilikua
yapata majira ya saa 6:48 usiku, haelewi nini afanye..!!
Akajaribu kukumbuka matukio ya siku hyo tangu asubuhi,
akakumbuka kitu ambacho kilimshtua kidogo!!
Akanyanyuka pale kitandani na kwenda katika meza ndogo
iliyokuwepo chumbani mle..akavuta droo yake na kutoa kibunda
cha pesa na kuanza kuhesabu.
Akagundua zilikua ni milioni moja na laki moja!! Akatafakari kwa
muda na kuishirikisha akili yake katika kufikiri, akajikuta
anaangua kilio!!.
★★★★★★★★★★★★★★
Don't Miss Episode 02

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni