RIWAYA: HISTORIA BATILI
MTUNZI & MWANADISHI:
Jumaa Khatib Mdharuba(Jk)
+255718274130
EPISODE O16
1⃣6⃣
★★★★★★★★★★★★★★★★
“Detective, nahitaji ripoti kuhusu ile kazi ambayo uliwa'assign' vijana wako Ahmed na Nuro” Rukia alisikia maneno haya baada ya kupokea simu yake ya mezani iliyokuwa inatoka kwa 'Boss'..Haikua kawaida ya Ally Ngoswe kupiga simu kuuliza juu ya kazi na kutaka ripoti kabla ya muda uliopangiwa kazi kuisha, jambo hili lilimshangaza sana Rukia, ingawa ilibidi awe na majibu tu sababu ndio mambo ya kazi..unafanya anachotaka boss, whether you like it or not!!.
“Unahitaji ripoti leo?” Aliamua kuuliza ingawa alijua kabisa kuwa hakutakua na jibu tofauti na 'Ndio'.
“Within these fifteen minutes” Ally aliweka msisitizo na kumfanya Rukia aanze kukuna kichwa pale ofisini kwake kama anayewashwa na nywele..
“Naomba unipe angalau siku mbili boss ili tukuletee ripoti kamili, maana Ahmed nimemuagiza akafuatilie zaidi ili aripoti kitu kilicho kamili, kwahiyo hivi tunavyoongea yupo Canada amemfuatilia Khatib..”
“Unasemaje wewe?? Umefikia hatua ya kumtuma mtu akafuatilie Canada bila kunipa taarifa? Yaani mtu mmoja tu huyo mnafikia hatua ya kumgharamia kiasi hicho kwa kutumia fedha za walipa kodi?” Ally alifoka katika simu, na kumfanya Rukia ambaye alikua upande wa pili achanganyikiwe..
“Nakuomba ofisini kwangu sasa hivi” Ndivyo alivyomalizia Ally na kukata simu..
Rukia alitoka katika ofisi yake ambayo ilikua ghorofa ya tatu katika jengo lile la ghorofa sita na moja kwa moja akaiendea lift na kupanda haraka hadi ghorofa ya tano ilipokua ofisi ya boss wake.. Akafungua mlango ule wa kioo ambao ulikua hauruhusu mtu kuona kinachoendelea ndani, kisha akazama ndani na moja kwa moja akajikaribisha kwenye kiti kilichokua mbele ya meza ya boss huku akimuangalia boss usoni ambaye mpaka sasa alikua bize amekodolea macho yake katika computer ya pale ofisini..
Rukia alibaki kimya, dakika tano zikapita, huku Ally akiwa bado anaonekana yuko busy na computer yake.
“Boss” Rukia aliamua kuvunja ukimya na kumfanya Ally ashtuke na kuanza kumuangalia Rukia..kisha akatoa tabasamu la kejeli baada ya kumuangalia sana Rukia ambaye hakuwa anajua hatma yake haswa itakua ni nini..
“Unapotka kufanya maamuzi kama hayo ni lazima unishirikishe, sio unajiamulia tu, chochote kitakachotokea ni mimi ndiye nitakayetakiwa kutoa majibu kwa mheshimiwa, na sio wewe..sasa wewe unajiamulia tu, huo ni ukosefu wa nidhamu ya kazi..au unataka kunambia umekua mwenyeji sasa? Umezoea kazi sio? Kwa miaka yako kumi kazini ndo unajiona unajua sana?” Rukia wakati huu wote alikua akiangalia vidole vyake akiwa amejiinamia..
“Hapana boss,naomba unisamehe nimekosea sikukwambia, ila ni mpango mzuri, na naamini tutafanikiwa katika hili”
“Acha kuongea upuuzi wewe Rukia, huo unaoongea hapo ni utumbo, acha kabisa kusema utafanikiwa kirahisi tu hivyo..acha kabisa” Ally Ngoswe alifoka kwa sauti ya juu sana huku akisimama kutoka pale kwenye kiti alipokua amekaa..
“Mpigie simu huyo Ahmed niongee nae” Ally aliagiza na Rukia akatekeleza. Baada ya simu kupokelewa Rukia alimueleza Ahmed kuwa boss anataka kuongea nae..
“Unashirikiana na Detective kufanya jambo la kipuuzi lisilo na maslahi yoyote kwa taifa letu, rudi huku haraka” Baada ya maneno haya Ally akamkabidhi simu Rukia ambaye aliweka sikioni na kumwambia Ahmed afanye kama alivyoambiwa na boss..kisha simu ikakatwa na kumfanya Ahmed apigwe na butwaa..
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Hisham alishangazwa na sms ile, akairudia kuisoma kwa mara ya pili na ya tatu..Jina la mtumaji likiwa limeseviwa kama SauKhat..akaanza kutafakari kwa kina sana juu ya mtumaji wa sms ile atakua ni nani hasa.. Ni kweli anafahamu kuwa SauKhat ni kampuni ya boss wake Khatib, lakini je, ni yeye ndiye amefanya hivyo? Au ni mmoja kati ya wafanyakazi wa kampuni ile? Akawa na maswali mengi sana ambayo hakuyapatia majibu, na hata alivyojibiwa e-mail na Khatib aliisoma lakini hakuelewa ameambiwa nini..! Akaisevu namba ya mtumaji wa sms ile kwenye simu yke kisha akaifuta ile sms kabla ya kurudisha simu kwa mkewe Regina..
“Umemaliza?” Regina aliuliza akipokea simu yake kutoka kwa Hisham.
“Done” Alijibu Hisham kwa kifupi.
******
Baada ya Hamida kupata nguvu aliruhusiwa kutoka kuja kujumuika na wenzake na pia kuona hali ya mwanae..
“Mwanangu anaendeleaje? Amepona Abdul?” Hamida alimuuliza mamaake mara tu baada ya kutoka pale nje..
“Ndio, yuko hapo chumbani anaendelea vizuri sana..” Nana alimjibu mwanae huku akimlaki kwa kumkumbatia..
“Ila Dokta kasema kwa sasa tumuache kwanza aendelee na mgonjwa tutaingia kumuona tena baadae..”
“Ok sawa mama, na damu amepata kwa nani? ”
“Yaani mwanangu tumshukuru sana Dokta Idd..baada ya kuona hali ya mgonjwa imekua mbaya aliamua kujitolea damu..kuna watu wana moyo wa huruma sana, Mungu amueke ili aweze kuwasaidia wengi zaidi..”
“Oooh..Alhamdulillah..yuko wapi huyo Dokta nikampe shukrani zangu kwa kuniokolea mwanangu?”
“Yupo hapo chumba cha Daktari namba mbili, ila kuna mgonjwa yuko nae, subiri mgonjwa akitoka utaingia..hana tatizo kabisa hyu Dokta ni mtu mzuri sana..” Nana alizidi 'kumfagilia' Dokta Idd Fauz na kumfanya Hamida azidi kupata hamu ya kumuona..
Baada ya mgonjwa kutoka, Hamida akaingia moja kwa moja chumba cha Dokta Idd..
“Asante sana Dokta, nimeambiwa wewe ndiye uliyejitolea damu kwa ajili ya Abdul, nakushukuru sana Dokta, hata sijui niielezee vipi furaha yangu kwa mtu mwenye moyo kama wewe..” Hamida alimimina rundo la shukrani kwa Dokta Idd..
“Mimi pia nina watoto, najua ni jinsi gani wazazi wanaumia wanapofikia katika wakati mgumu kuhusu watoto wao kama hivi..”
Dokta Idd ambaye kwa Nana na Hamida alionekana kuwa zaidi ya shujaa aliongea mengi sana na Hamida, maisha ambayo Hamida alipitia kuhusu mwanae yule Abdul na mambo mengi yaliyotokea mpaka kutengana na babaake..Ila Hamida hakutaka kuweka wazi juu ya nani haswa ndio babaake Abdul, kwani kwa kufanya hivyo kungemfanya Dokta Idd akose uhuru wa kutoa msaada siku zingine..kwani kwa muda huu Khatib hakuwa na jina zuri sana kwenye jamii..wapo waliomuamini na wapo ambao hawakua na imani naye hata kidogo..
Baadae wakaagana.. Huku kila mmoja akichukua namba ya simu ya mwenzie..
******
Siku ile Abdul hakupata ruhusa ya kurudi nyumbani..hivyo kufanya Jioni ile Hisham na Regina waondoke kurudi nyumbani baada ya kuridhishwa na maendeleo ya mtoto..wakiamini kesho yake lazima angeruhusiwa..
Hamida alibaki hospitali na mtoto, Nana akarudi nyumbani kuwatayarishia chakula..
Siku ya pili wakaruhusiwa kuondoka.
*****************************
Mawasiliano kati ya Dokta Idd na Hamida, mara nyingi wakipigiana simu na kutumiana sms wakiulzana kuhusu mambo yao ya kila siku ya kimaisha..ingawa siku zote Hamida hakuacha kumsifia Dokta Idd kwa jinsi alivyo na moyo wake wa imani..na roho iliyojaa huruma..
Hadi hapo siku moja ambapo Hamida alimpigia simu Dr Idd..
“Kuna kitu nataka nikwambie Dokta”
“Nakusikiliza mama Abdul”
“Mmmh hata sijui naanzia wapi..ilaa..mmhh..basi ngoja nkutumie sms”
“Mmh haya kama umeshindwa kuongea, naisubiri hiyo sms”
Hamida akakata simu kisha akaandika sms haraka haraka kabla ya kuituma kwa Dokta Idd..
Dokta Idd alipigwa na butwaa baada ya
kusoma sms ile ambayo ilisomeka “Nahisi nimeanza kupata hisia za mapenzi juu yako Dokta”
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Baada ya wiki mbili, Khatib alimpigia simu mamaake na kumwambia yuko njiani anarudi nyumbani Tanzania..
“Sasa kuhusu yule Nana na yule mwanawe ambaye tuliongea siku ile baada ya mimi kutoka pale Hospitali, hujanijibu bado..” Mama Mdharuba aliulizia juu ya jambo ambalo walilijadili siku ile baada ya kupewa taarifa na Hisham na kumpigia simu mamaake ambaye aliuliza ni nini hasa kimetokea..
“Mama, naomba unisubiri mpaka nifike halafu tutaongea vizuri”
“Hapana, wewe nambie tu kabisa kama kweli unamtaka yule Hamida na mwanae uishi nao ili mimi nitengeneze mazingira kabla hujafika huku, mpaka ukifika kila kitu kimeshakua sawa..”
“Sawa basi mama, wewe nirudishie Hamida..maana kwa sasa ndiye mtu pekee wa kuishi nae, ili pia niwe na mwanangu karibu” Khatib aliamua kukubaliana na wazo la mamaake la kuwaweka pamoja tena yeye na Hamida..
“Safi sana mwanangu, maana yule bibi yake Abdul ashaanza kuonekana kuwa kiherehere..”
Baada ya kumaliza maongezi haya, Mama Mdharuba alibofya bofya tena simu kisha akaweka sikioni..
“Haloo Sheikh Lesangwa, za siku?” Ndivyo alivyoanza maongezi baada ya kuonekana kuwa upande wa pili ameanza kuongea..
“Mimi mzima, sasaa..unamkumbuka yule mwanangu alokupigia simu siku ile kuhusu lile jambo lake?” Aliuliza swali Mama Mdharuba kisha akaweka nukta kidogo kabla ya kuendelea..
“Ana jambo lake jingine dogo nataka umtengenezee..”
★★★★★★★★★★★★★★★★
Let's call it a day..
Ndo kwanzaaa tunaanza..
Episode 017 coming soon..
Whatsapp↘
+255718274130
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni